KWA UFUPi, Simulizi La IMBORI NA MAYO.
Ndo limefanya kukawa na Mashindano haya. š» Kuna Baadhi ya Marafiki zangu hawafahamu Kwamba kuna Tamasha la Imbori, Mwaka 2018 Mimi nilishiriki ili Kuwania Nafasi ya Ushindi kulipata Taji la MR. MAYO š. Niliambulia Nafasi Ya III. š¤¦š½āāļø * Ila Ilinifaa. #___ Basi Niliifupisha Stori Ya Imbori na Mayo kama Ifuatavyo, ššš #IMBORI ni binti Mrembo kutoka Kabila la Kiiraqw aliyeishi Miaka takribani 400 iliyopita!š¤¤š¤¤ Binti huyu aliwavutia Vijana wa Kiume hasa Mayo kutokana Uremboš§ na Mvuto wake wa kipekee! Ndipo Yalipoanza mahusiano yakeš¤ na kijana Mayo hadi kupelekea Imbori kupata Mimba kabla ya kuolewaš¬ kitendo ambacho ni ukiukwaji wa Mila na desturi za Kabila la kiiraqw. Vijana hawa Walipaswa kukabiliwa na Adhabu iliyoamriwa na Baraza la wazee, ya Binti kutoswa Kwenye Msitu wenye Wanyama waKali š„š¢š¢lakini Mayo aliitoroka Adhabu ya Viboko na Kutokomea Wasipopafahamu!. Kwa Msaada wa Mungu na Kwa ujasiri na Werevu Aliojaliwa Mayo alimnasua Imbori aliyetoswa kwenye Msitu wenye Wanyama wakali na kuishi naye sehemu iliyokua salama karibu na Makazi ya Jamii zingine (wabarbaig). Baada ya Miaka 6 Ndugu na Wanajamii ya Kiiraqw Walipata Taarifa za kuwashtua na kuwafanya waogope Mno š², ....
š Okay!
Sasa Ikawa Hiviii, baada ya Muda Wa Miaka kadhaa kupita familia ya MAYO na Imbori iligundulika kwamba Inaishi.
Hiyo ilikua baada ya Ndugu zao kuwaona bila kuamini mara kadhaa walipo safiri wakati wa Biashara za Mabadilishano kwa wakati huo.
Basi wakapanga kukutana Nao, ndipo Mayo na Imbori wakaomba Msamaha kwa jamii na Wakaomba toba kwa Mungu. Jamii kupitia Baraza la Wazee iliridhia Msamaha. Na kuwaozesha vijana Wao kihalali.
Sasa lile swala la NYAKATI ZA MABADILIKO NDIO LINAINGIA HAPA.
#Wazee walijitafakari na wakatambua kwamba ile ilikua ishara ya Mungu Kwa Kuwanusuru Mayo na Imbori ambao wana Watoto wawili sasa, Wazee wa Baraza walikiri kwamba Mungu hakupendezwa na Adhabu hiyo wakazitathimini upya sheria zao na Kuzibadilisha.
Basi jamii ya Kabila la Kiiraqw ikafikia Nyakati za Mabadiliko ambapo kufikia leo Msamaha hutolewa na Wazazi kwa Vijana wao walioteleza dhambini na wakatambua pia wakakiri makosa yao na Kuomba kuomba Toba kwa Mungu.
Lakini Pia Jamii kwa Ujumla ikisimamia Maadili ya vijana Kupitia wasimamizi kama Vile wazazi, serikali na Taasisi za Dini ili kuwaepusha na Athari za Ukosefu wa Maadili.
.
Kuhusu Imbori na Mayo wakarudi kuishi Katika Makazi yao Ambayo sasa ndugu zao waliitambua kama Mji wa Kina Imbori wakauita "Aya Imbori" (kiswahili Mtaa Wa Imbori)
Na hatimaye likatoholewa hadi likaasisiwa jina La Mbulu inayotambulika kama Wilaya sasa!
Ni vizuri hivo, bora hata kuna Tamasha kama hilo linafanyikaga wapi?